Jumanne, 7 Juni 2016

KIFO CHA MUHAMMAD ALI CHAZUA SIASA MAREKANI

Kifo cha muhammad ali kimezua malumbano makali katika ulingo wa kisiasa miongoni mwa wagombea wa kiti cha uraisi katika uchaguzi mkuu,utakaofanyika mwezi novemba nchini marekani.


Katika risala zake za rambirambi mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Republican Donald trump,amesema kuwa Ali kwa hakika alikuwa bingwa ambaye atakumbukwa na wengi mwaka jana ,Ali alilaani wito uliotolewa na bwana trump ya kuwazuia kabisa waislamu kuingia  nchini marekani.


Kwa upande wake mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya
chama cha Democratic Senetor  Bernie sanders amemshutumu Bwana  trump na kumtaja  kuwa mnafiki.


Naye bi Hillary clinton amesema kuwa bwana trump anafaa kuhukumiwa kwa matamshi yake anayotoa.


Bondia huyo alifariki siku ya ijumaa huko Arizona,na alikuwa akiugua maradhi ya kusahau sahau,kwa zaidi ya mwaka 30.

KIFO CHA MUHAMMAD ALI CHAZUA SIASA MAREKANI

RC AAGIZA MKURUGENZI HANANG AFIKISHA MAHAKAMANI

Mkuu wa mkoa manyara dr Joel bendera ameagiza aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Hanang,Felix mabula na aliyekuwa muweka hazina wa halmashauri hiyo Matonya mzengo wafikishwe mahakamani kujibu mashtaka ya upotevu wa sh 932 milioni.


Akuzungumza juzi wilayani Hanang Dr Bendera alisema taarifa ya uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha ziliokuwa zinawakabili Mabula na Mizengo waliosimamishwa tangu april 6 mwaka,zimewaingiza hatianiani.


Dr Bendera alisema kamati hiyo ilibaini kuwa Mabula na Matonya wameisababishia halmashauri hiyo madeni ikiwemo hospitali ya wilaya(Tumaini) inayodaiwa na bohari ya dawa(MSD) sh34.606 milioni,hivyo wamepoteza sifa za utumishi wamefikishwa mahakamani.

POLISI WATAKA USHIRIKIANO KUTHIBITI UHALIFU MWANZA

Kamanda wa polisi wa mkoa wa mwanza Ahmed msangi amesema vyombo vya dola pekee haviwezi kupigana vita dhidi ya uhalifu bila ya kuwepo ushirikiano na wadau wengine.


Msangi alisema hayo wakati chama cha waandishi wa habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania (ojadaet),kilipokuwa kinazindua kampeni ya kupinga vitendo hivyo.


"Amani,utulivu ni bidhaa adimu,tushirikiane kuona mkoa wetu unakuwa salama,maana hata uwekezaji hawezi kuwekeza katika sehemu ambayo siyo salama,hivyo kuendelea kutokea uhalifu ni kuwaogopesha,na kukwamisha maendeleo".alisema msangi

AUAWA KWA KUPORA SIMU

Mtu mmoja ameuawa kwa kipigo cha kuchomwa moto kwa tuhuma ya kupora simu ya mkononi aina ys tecno.


Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza Ahmed msangi alisema juni 2 mtu huyo ambaye jina halikupatikana anaekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 hadi 35,aliuawa baada ya kumpora simu mpitanjia eneo la Ngaza kata ya Nyegezi jijini hapo.


"Kabla ya kupora simu,mtu aliyejulikana kwa jina la Aanica rwezaura alitishiwa na yule aliyeuawa kwa panga lakini wananchi wenye hasira kali walimwandama,kumpiga na hatimaye kumchoma moto hadi kufa".alisema kamanda msangi

WANAFUNZI 130 WA CHUO KIKUU CHA TUMAINI TAWI LA MBEYA KUTOFANYA MTIHANI WA MWISHO KWA KUKOSA USAJILI WA NACTE

Zaidi ya wanafunzi 130 wanaosoma kozi ya afya ya jamii katika chuo kikuu cha Tumaini mikumira tawi la mbeya wako hatarini kutofanya mitihani yao ya mwisho baada ya uongozi wa chuo hicho kushindwa kukamilisha taratibu za kuwasajili kwa wakati kwenye baraza la taifa la elimu ya ufundi,NACTE.


Wanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini makumira tawi la mbeya ambao wamebakiza mwezi mmoja kuhitimu elimu yao ya chuoni hapo,wamekusanyika mbele ya majengo ya utawala wa chuo hicho na kupaza sauti zao wakitaka kujua hatma yao kuhusu usajili wao katika baraza la taifa la elimu ya ufundi,NACTE.


Kutokana na kutokuwa na uhakika wa kuhitimu elimu yao kwa amani,wanafunzi hao wamesikitishwa na uongozi wa chuo hicho kinachomilikiwa na kanisa kwa vitendo wanavyifanyiwa,hivyo wakaiomba serikali kuingia kati ili waweze kutendewa haki.

BAADHI WAACHIWA TUHUMA ZA MAUAJI MSIKITINI

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ahmed msangi amesema pamoja na kuwaachia watu ambao hakutaja idadi yao,bado wanafuatulia wengine ambao wanaonekana kuhusika na tukio hilo,bila kutaja idadi ya watu walioachiwa.


"Wapo baadhi walioachiwa,wengine watafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya kuona ushahidi una kila aina ya dalili za kuhusika na tukio hilo".amesema msangi


Katika mauaji hayo,watu watatu waliuawa kwa kukatwa mapanga wakisali msikitini akiwemo imamu wa msikiti huo,Feruz ismail na wengine wawili na kumjeruhi mtoto wa miaka 13.