Chama cha siasa cha ACT-wazalendo nchini Tanzania kimesema kuwa kinakusudia mikutano ya hadhara katika miji mikubwa nchini kwa kushirikiana na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA,kuongea na wananchi juu ya wabunge waliotolewa nje ya bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Tamko hilo limetolewa jana jijini Dar- es-salam na katibu mwenezi wa chama cha ACT-wazalendo Sabini Richard wakati akiongea na waandishi w habari jijini Dar-es-salaam juu ya hatua iliyochukuliwa na chama hicho kufuatia kutoridhishwa na mwenendo wa bunge kidemokrasia.
Mikutano hiyo inatarajiwa kuanzia jijini Dar-es-salaam na baadae kuelekea sehemu mbali mbali katika miji mimgine mikubwa nchini Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni