Mkuu wa mkoa wa Arusha Felix Ntibenda amesema kuanzia wiki ijayo tatizo la sukari litakuwa historia,kwani viwanda vya sukari vya ndani vinaanza uzalishaji,Ntibenda alisema hayo wakati akikabidhi mradi wa ufugaji kuku wa kienyeji na mbuzi wa maziwa katika kata ya Muriel eneo la kwa mrombo unaoendeshwa na mfuko wa maendeleo ya jamii( TASAF).
"Hivi sasa wananchi mnauziwa sukari kilo moja kwa shilingi 2,500 hadi 3,500 kwa kilo moja,lakini sasa tunasema sukari itapatikana kuanzia wiki ijayo na wanaofunga Ramadhan wasiwe na shaka,watapata sukari".alisema
Meya wa jiji la Arusha,Calist Lazaro amesema anaungana na serikali kuhakikisha maendeleo ya jiji la Arusha yatapatikana ikiwemo ukusanyaji wa bodi za majengo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni