Diamond platinumz alisema haya kwenye kipindi cha FNL amesema kitendo akichofanya Wema kupost kazi zake anadhani imefika wakati labda Wema Sepetu ameona hakuna sababu ya yeye kuendelea kumchukia Diamond platinumz na ndiyo maana ameonyesha upendo kwa kusapoti kazi zake na za wasanii kutoka kwenye lebo yake.
"Kuna wakati inafika watu mnakuwa mmekuwa labda,mtu anaona hana sababu ya kuendelea kukuchukia au kuwa na vita na wewe,sababu mwanzo mkiwa bado mnaenda mnaona kuna vitu mko navyo ndiyo maana kuna kuwa na chuki kubwa,lakini ikifika wakati kila mtu amesonga mbele na maisha yake,ameridhika na naisha yake anaona kwanini nimuwekee vita mtu fulani hivyo anadhani labda wakati huo ndiyo huu maana mwenyewe nimeona kweli amepost
BET,amepost promo ya Rich mavoko kwangu mimi nafurahi kwasababu naona haina faida kwa sisi wasanii kuwekeana vita". alisema Diamond
Mbali na hilo Diamond platinumz alidai toka ameachana na Wema sepetu hana namba yake ya simu,hajawahi hata siku moja kumpigia simu wala Wema sepetu hajawahi kumpigia simu Diamond platinumz.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni