Kifo cha muhammad ali kimezua malumbano makali katika ulingo wa kisiasa miongoni mwa wagombea wa kiti cha uraisi katika uchaguzi mkuu,utakaofanyika mwezi novemba nchini marekani.
Katika risala zake za rambirambi mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Republican Donald trump,amesema kuwa Ali kwa hakika alikuwa bingwa ambaye atakumbukwa na wengi mwaka jana ,Ali alilaani wito uliotolewa na bwana trump ya kuwazuia kabisa waislamu kuingia nchini marekani.
Kwa upande wake mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya
chama cha Democratic Senetor Bernie sanders amemshutumu Bwana trump na kumtaja kuwa mnafiki.
Naye bi Hillary clinton amesema kuwa bwana trump anafaa kuhukumiwa kwa matamshi yake anayotoa.
Bondia huyo alifariki siku ya ijumaa huko Arizona,na alikuwa akiugua maradhi ya kusahau sahau,kwa zaidi ya mwaka 30.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni